18Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami nawatuma vivyo hivyo.
19Kwa ajili yao najiweka wakfu ili wao nao wapate kutakaswa katika ile kweli.
20“Siwaombei hawa peke yao, bali nawaombea na wale wote watakaoniamini kupitia neno lao
21ili wawe na umoja kama vile wewe Baba ulivyo ndani yangu na mimi nilivyo ndani yako, wao nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kuamini ya kuwa wewe ndiye uliyenituma mimi.
22Utukufu ule ulionipa nimewapa wao, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja.