26Yesu akamwambia, “Mimi ninayezungumza nawe, ndiye.”
27Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kumwona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemuuliza, “Unataka nini kwake?” Au “Kwa nini unazungumza naye?”
28Yule mwanamke akaacha mtungi wake, akarudi mjini akawaambia watu,
29“Njooni mkamwone mtu aliyeniambia kila kitu nilichotenda! Je, yawezekana huyu ndiye Kristo?”
30Basi wakamiminika watu kutoka mjini wakamwendea Yesu.