1Baada ya haya, Yesu alikwenda ngʼambo ya Bahari ya Galilaya, ambayo pia huitwa Bahari ya Tiberia.
2Umati mkubwa wa watu uliendelea kumfuata, kwa sababu waliona ishara nyingi za miujiza alizofanya kwa wagonjwa.
3Kisha Yesu akapanda mlimani akaketi huko pamoja na wanafunzi wake.
4Pasaka ya Wayahudi ilikuwa imekaribia.