Yohana 6

Yesu alipotazama na kuuona ule umati mkubwa wa watu ukimjia, akamwambia Filipo, “Tutanunua wapi mikate ili watu hawa wale?”

John 6:5 (UKJV) When Jesus then lifted up his eyes, and saw a great company come unto him, he says unto Philip, Whence shall we buy bread, that these may eat?

3Kisha Yesu akapanda mlimani akaketi huko pamoja na wanafunzi wake.

4Pasaka ya Wayahudi ilikuwa imekaribia.

5Yesu alipotazama na kuuona ule umati mkubwa wa watu ukimjia, akamwambia Filipo, “Tutanunua wapi mikate ili watu hawa wale?”

6Aliuliza swali hili kumpima, kwa maana alishajua la kufanya.

7Filipo akamjibu, “Hata fedha kiasi cha dinari mia mbili, hazitoshi kununua mikate ya kuwapa watu hawa ili kila mtu apate kidogo.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.