66Tangu wakati huo wafuasi wake wengi wakarejea nyuma wakaacha kumfuata.
67Hivyo Yesu akawauliza wale wanafunzi wake kumi na wawili, “Je, ninyi pia mnataka kuondoka?”
68Simoni Petro akamjibu, “Bwana, tuondoke twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
69Tunaamini na kujua kuwa wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu.”
70Ndipo Yesu akajibu, “Je, sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Lakini mmoja wenu ni ibilisi.”