Yohana 8

Hivyo Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli.

John 8:36 (UKJV) If the Son therefore shall make you free, all of you shall be free indeed.

34Yesu akajibu, “Amin, amin nawaambia, kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.

35Mtumwa hakai nyumbani anakotumika siku zote, lakini mwana hukaa nyumbani daima.

36Hivyo Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli.

37Ninajua ya kuwa ninyi ni wazao wa Abrahamu, lakini mnatafuta wasaa wa kuniua kwa sababu ndani yenu hamna nafasi ya neno langu.

38Ninasema yale niliyoyaona mbele za Baba yangu, nanyi inawapa kufanya yale mliyosikia kutoka kwa baba yenu.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.