Yohana 9

Tangu zamani hatujasikia kwamba mtu amemponya yeyote aliyezaliwa kipofu.

John 9:32 (UKJV) Since the world began was it not heard that any man opened the eyes of one that was born blind.

30Yule mtu akawajibu, “Hili ni jambo la ajabu! Hamjui anakotoka, naye amenifungua macho yangu!

31Tunajua ya kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomcha na kumtii.

32Tangu zamani hatujasikia kwamba mtu amemponya yeyote aliyezaliwa kipofu.

33Kama huyu mtu hakutoka kwa Mungu, asingeweza kufanya lolote.”

34Wao wakamjibu, “Wewe ulizaliwa katika dhambi kabisa, nawe unajaribu kutufundisha?” Wakamfukuza atoke nje.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.