Yoshua 4

“Chagua watu kumi na wawili miongoni mwa watu, kila kabila mtu mmoja,

Joshua 4:2 (UKJV) Take you twelve men out of the people, out of every tribe a man,

1Wakati taifa lote lilipokwisha kuvuka Mto Yordani, Bwana akamwambia Yoshua,

2“Chagua watu kumi na wawili miongoni mwa watu, kila kabila mtu mmoja,

3nawe uwaambie wachukue mawe kumi na mawili katikati ya Mto Yordani, palepale makuhani waliposimama, wayachukue na kuyaweka mahali mtakapokaa usiku huu wa leo.”

4Basi Yoshua akawaita watu kumi na wawili ambao alikuwa amewachagua kutoka miongoni mwa Waisraeli, mtu mmoja kutoka kila kabila,

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.