Waamuzi 5

Watu wa Zabuloni walihatarisha maisha yao, vilevile nao watu wa Naftali.

Judges 5:18 (UKJV) Zebulun and Naphtali were a people that jeopardized their lives unto the death in the high places of the field.

16Kwa nini ulikaa katikati ya mazizi ya kondoo kusikiliza sauti ya filimbi zinazoita makundi? Kwa jamaa za Reubeni, palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni.

17Gileadi alikaa ngʼambo ya Yordani. Naye Dani, kwa nini alikaa kwenye merikebu siku nyingi? Asheri alikaa kwa utulivu ufuoni mwa bahari, akikaa kwenye ghuba zake ndogo.

18Watu wa Zabuloni walihatarisha maisha yao, vilevile nao watu wa Naftali.

19“Wafalme walikuja na kufanya vita; wafalme wa Kanaani walipigana huko Taanaki karibu na maji ya Megido, lakini hawakuchukua fedha wala nyara.

20Kutoka mbinguni nyota zilipigana, nyota kutoka njia zake zilipigana na Sisera.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.