28Usimchinje ngʼombe na ndama wake, au kondoo na kitoto chake siku moja.
29“Unapomtolea Bwana dhabihu ya shukrani, itoe kwa namna ambayo itakubalika kwa niaba yako.
30Ni lazima iliwe siku iyo hiyo, pasipo kubakiza chochote mpaka asubuhi. Mimi ndimi Bwana.
31“Shikeni maagizo yangu na kuyafuata. Mimi ndimi Bwana.
32Msilinajisi Jina langu takatifu. Lazima nikubalike kuwa mtakatifu kwa Waisraeli. Mimi ndimi Bwana ninayewafanya watakatifu,