42akapaza sauti kwa nguvu akasema, “Umebarikiwa wewe miongoni mwa wanawake, naye mtoto utakayemzaa amebarikiwa.
43Lakini ni kwa nini mimi nimepata upendeleo kiasi hiki, hata mama wa Bwana wangu afike kwangu?
44Mara tu niliposikia sauti ya salamu yako, mtoto aliyeko tumboni mwangu aliruka kwa furaha.
45Amebarikiwa yeye aliyeamini kwamba lile Bwana alilomwambia litatimizwa.”
46Naye Maria akasema: “Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,