52Amewashusha watawala toka kwenye viti vyao vya enzi, lakini amewainua wanyenyekevu.
53Amewashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri, bali matajiri amewafukuza mikono mitupu.
54Amemsaidia mtumishi wake Israeli, kwa kukumbuka ahadi yake ya kumrehemu
55Abrahamu na uzao wake milele, kama alivyowaahidi baba zetu.”
56Maria akakaa na Elizabeti karibu miezi mitatu, kisha akarudi nyumbani kwake.