55Abrahamu na uzao wake milele, kama alivyowaahidi baba zetu.”
56Maria akakaa na Elizabeti karibu miezi mitatu, kisha akarudi nyumbani kwake.
57Ulipowadia wakati wa Elizabeti kujifungua, alizaa mtoto mwanaume.
58Majirani zake na jamii zake wakasikia jinsi Bwana alivyomfanyia rehema kuu, nao wakafurahi pamoja naye.
59Siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto, wakataka yule mtoto aitwe Zekaria, ambalo ndilo jina la baba yake.