Luka 13

Yesu akauliza tena, “Nitaufananisha Ufalme wa Mungu na nini?

Luke 13:20 (UKJV) And again he said, Unto which shall I liken the kingdom of God?

18Kisha Yesu akauliza, “Ufalme wa Mungu unafanana na nini? Nitaufananisha na nini?

19Umefanana na punje ya haradali ambayo mtu aliichukua na kuipanda katika shamba lake. Nayo ikakua, ikawa mti nao ndege wa angani wakatengeneza viota vyao kwenye matawi yake.”

20Yesu akauliza tena, “Nitaufananisha Ufalme wa Mungu na nini?

21Unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua akaichanganya katika kiasi kikubwa cha unga mpaka wote ukaumuka.”

22Yesu akapita katika miji na vijiji, akifundisha wakati alisafiri kwenda Yerusalemu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.