20Yesu akauliza tena, “Nitaufananisha Ufalme wa Mungu na nini?
21Unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua akaichanganya katika kiasi kikubwa cha unga mpaka wote ukaumuka.”
22Yesu akapita katika miji na vijiji, akifundisha wakati alisafiri kwenda Yerusalemu.
23Mtu mmoja akamuuliza, “Bwana, ni watu wachache tu watakaookolewa?”
24Yesu akawaambia, “Jitahidini sana kuingia kupitia mlango mwembamba, kwa maana nawaambia wengi watajaribu kuingia, lakini hawataweza.