41Kisha Yesu akawaambia, “Imekuwaje basi wao husema Kristo ni Mwana wa Daudi?
42Daudi mwenyewe anasema katika Kitabu cha Zaburi: “ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume,
43hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.” ’
44Ikiwa Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ basi atakuwaje mwanawe?”
45Wakati watu wote walikuwa wanamsikiliza, Yesu akawaambia wanafunzi wake,