42Daudi mwenyewe anasema katika Kitabu cha Zaburi: “ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume,
43hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.” ’
44Ikiwa Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ basi atakuwaje mwanawe?”
45Wakati watu wote walikuwa wanamsikiliza, Yesu akawaambia wanafunzi wake,
46“Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kukaa kwenye nafasi za heshima katika karamu.