25Yesu akawaambia, “Ninyi ni wajinga kiasi gani, nanyi ni wazito mioyoni mwenu kuamini mambo yote yaliyonenwa na manabii!
26Je, haikumpasa Kristo kuteswa kwa njia hiyo na kisha aingie katika utukufu wake?”
27Naye akianzia na Sheria ya Mose na Manabii wote, akawafafanulia jinsi Maandiko yalivyosema kumhusu yeye.
28Nao walipokaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, Yesu akawa kama anaendelea mbele.
29Lakini wao wakamsihi sana akae nao, wakisema, “Kaa hapa nasi, kwa maana sasa ni jioni na usiku unaingia.” Basi akaingia ndani kukaa nao.