40Aliposema haya, akawaonyesha mikono na miguu yake.
41Wakashindwa kuamini kwa ajili ya furaha na mshangao waliokuwa nao. Akawauliza, “Mna chakula chochote hapa?”
42Wakampa kipande cha samaki aliyeokwa,
43naye akakichukua na kukila mbele yao.
44Akawaambia, “Haya ndiyo yale niliyowaambia nilipokuwa bado niko pamoja nanyi, kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika Sheria ya Mose, Manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.”