42Wakampa kipande cha samaki aliyeokwa,
43naye akakichukua na kukila mbele yao.
44Akawaambia, “Haya ndiyo yale niliyowaambia nilipokuwa bado niko pamoja nanyi, kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika Sheria ya Mose, Manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.”
45Ndipo akafungua fahamu zao ili waweze kuyaelewa Maandiko.
46Akawaambia, “Haya ndiyo yaliyoandikwa: Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu.