49“Tazama nitawatumia ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini hadi mtakapovikwa uwezo utokao juu.”
50Akiisha kuwaongoza mpaka kwenye viunga vya Bethania, akainua mikono yake juu na kuwabariki.
51Alipokuwa anawabariki, akawaacha, akachukuliwa mbinguni.
52Kisha wakamwabudu na kurudi Yerusalemu wakiwa wamejawa na furaha kuu.
53Nao wakadumu ndani ya Hekalu wakimtukuza Mungu. Amen.