7Hivyo ikiwa utanisujudia na kuniabudu, vyote vitakuwa vyako.”
8Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mwabudu Bwana Mungu wako na umtumikie yeye peke yake.’ ”
9Kisha ibilisi akampeleka mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu, akamwambia, “Kama wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini kutoka hapa,
10kwa maana imeandikwa: “ ‘Atakuagizia malaika zake ili wakulinde;
11nao watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’ ”