Luka 6

Yuda mwana wa Yakobo, na Yuda Iskariote ambaye alikuwa msaliti.

Luke 6:16 (UKJV) And Judas the brother of James, and Judas Iscariot, which also was the traitor.

14Simoni aliyemwita Petro, Andrea nduguye, Yakobo, Yohana, Filipo, Bartholomayo,

15Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni aliyeitwa Zelote,

16Yuda mwana wa Yakobo, na Yuda Iskariote ambaye alikuwa msaliti.

17Akashuka pamoja nao, akasimama mahali penye uwanja tambarare. Hapo palikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wake na umati mkubwa wa watu kutoka sehemu zote za Uyahudi, kutoka Yerusalemu, na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni.

18Walikuwa wamekuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Wale waliokuwa wakiteswa na pepo wachafu akawaponya.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.