15Yeyote aliye juu ya dari ya nyumba asishuke au kuingia ndani ili kuchukua chochote.
16Aliye shambani asirudi nyumbani kuchukua vazi lake.
17Ole wao wenye mimba na wale wanaonyonyesha watoto siku hizo!
18Ombeni mambo haya yasitokee wakati wa baridi.
19Kwa maana siku hizo zitakuwa za dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo, hapo Mungu alipoumba ulimwengu, mpaka leo, na wala haitakuwako tena kamwe.