33Jihadharini! Kesheni! Kwa maana hamjui wakati ule utakapowadia.
34Ni kama mtu anayesafiri. Anaiacha nyumba yake na kuwaachia watumishi wake kuiangalia, kila mtu na kazi yake, kisha akamwamuru yule bawabu aliye mlangoni akeshe.
35“Basi kesheni kwa sababu hamjui ni lini mwenye nyumba atakaporudi: iwapo ni jioni, au ni usiku wa manane, au alfajiri awikapo jogoo, au mapambazuko.
36Kama akija ghafula, asije akawakuta mmelala.
37Lile ninalowaambia ninyi, nawaambia watu wote: ‘Kesheni!’ ”