11Kila mara pepo wachafu walipomwona, walianguka chini mbele yake na kupiga kelele wakisema, “Wewe ndiwe Mwana wa Mungu.”
12Lakini aliwaonya wasimseme yeye ni nani.
13Yesu akapanda mlimani na kuwaita wale aliowataka, nao wakamjia.
14Akawachagua kumi na wawili, ambao aliwaita mitume, ili wapate kuwa pamoja naye, na awatume kwenda kuhubiri
15na kuwa na mamlaka ya kutoa pepo wachafu.