Marko 4

Udongo huifanya iote kuwa mche, halafu suke, kisha nafaka kamili kwenye suke.

Mark 4:28 (UKJV) For the earth brings forth fruit of herself; first the blade, then the ear, after that the full corn in the ear.

26Pia akawaambia, “Ufalme wa Mungu unafanana na mtu apandaye mbegu shambani.

27Akiisha kuzipanda, usiku na mchana, akiwa amelala au ameamka, mbegu huota na kukua pasipo yeye kujua ikuavyo.

28Udongo huifanya iote kuwa mche, halafu suke, kisha nafaka kamili kwenye suke.

29Lakini nafaka inapokuwa imekomaa, mara mkulima huingia shambani na mundu wa kuvunia, maana mavuno yamekuwa tayari.”

30Akawaambia tena, “Tuufananishe Ufalme wa Mungu na nini? Au tutumie mfano gani ili kuueleza?

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.