6Lakini afadhali mshike njia kuwaendea kondoo wa nyumba ya Israeli waliopotea.
7Wakati mnapokwenda, hubirini mkisema, ‘Ufalme wa Mbinguni umekaribia.’
8Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo wachafu. Mmepata bure, toeni bure.
9Msichukue dhahabu, wala fedha, wala shaba kwenye vifuko vyenu.
10Msichukue mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala jozi ya pili ya viatu, wala fimbo, kwa maana mtendakazi anastahili posho yake.