Mathayo 12

Hatagombana wala hatapiga kelele, wala hakuna atakayesikia sauti yake njiani.

Matthew 12:19 (UKJV) He shall not strive, nor cry; neither shall any man hear his voice in the streets.

17Hii ilikuwa ili litimie lile neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kusema:

18“Tazama mtumishi wangu niliyemchagua, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. Nitaweka Roho wangu juu yake, naye atatangaza haki kwa mataifa.

19Hatagombana wala hatapiga kelele, wala hakuna atakayesikia sauti yake njiani.

20Mwanzi uliopondeka hatauvunja, na utambi unaofuka moshi hatauzima, mpaka atakapoifanya haki ishinde.

21Katika Jina lake mataifa wataweka tumaini lao.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.