19Hatagombana wala hatapiga kelele, wala hakuna atakayesikia sauti yake njiani.
20Mwanzi uliopondeka hatauvunja, na utambi unaofuka moshi hatauzima, mpaka atakapoifanya haki ishinde.
21Katika Jina lake mataifa wataweka tumaini lao.”
22Kisha wakamletea mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, na alikuwa kipofu na bubu. Yesu akamponya, hata akaweza kusema na kuona.
23Watu wote wakashangaa na kusema, “Je, yawezekana huyu ndiye Mwana wa Daudi?”