7Ninyi wanafiki! Isaya alikuwa sawa alipotabiri juu yenu kwamba:
8“ ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami.
9Huniabudu bure; nayo mafundisho yao ni maagizo ya wanadamu tu.’ ”
10Yesu akaita ule umati wa watu, akawaambia, “Sikilizeni na mwelewe:
11kinachomfanya mtu kuwa najisi mbele za Mungu si kile kiingiacho kinywani mwake, bali ni kile kitokacho kinywani mwake.”