18Lakini Yesu, akijua makusudi yao mabaya, akawaambia, “Enyi wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega?
19Nionyesheni hiyo sarafu inayotumika kwa kulipia kodi.” Wakamletea dinari.
20Naye akawauliza, “Sura hii ni ya nani? Na maandishi haya ni ya nani?”
21Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.” Basi Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.”
22Waliposikia hili, wakashangaa. Hivyo wakamwacha, wakaenda zao.