11Watatokea manabii wengi wa uongo, nao watawadanganya watu wengi.
12Kwa sababu ya kuongezeka kwa uovu upendo wa watu wengi utapoa,
13lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ataokolewa.
14Injili ya Ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo mwisho utakapokuja.
15“Hivyo mtakapoona lile ‘chukizo la uharibifu’ lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu (asomaye na afahamu),