Mathayo 24

Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo.

Matthew 24:46 (UKJV) Blessed is that servant, whom his lord when he comes shall find so doing.

44Kwa hiyo ninyi pia hamna budi kuwa tayari, kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja saa msiyotazamia.

45“Ni nani basi aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake amemweka kusimamia watumishi wengine katika nyumba yake, ili awape chakula chao kwa wakati unaofaa?

46Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo.

47Amin, nawaambia, atamweka mtumishi huyo kuwa msimamizi wa mali yake yote.

48Lakini kama huyo mtumishi ni mwovu, naye akasema moyoni mwake, ‘Bwana wangu atakawia muda mrefu,’

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.