4lakini wale wenye busara walichukua taa zao na mafuta ya akiba kwenye vyombo.
5Bwana arusi alipokawia kuja wale wanawali wote wakasinzia na kulala.
6“Usiku wa manane pakawa na kelele: ‘Tazameni, huyu hapa bwana arusi! Tokeni nje mkamlaki!’
7“Ndipo wale wanawali wote wakaamka na kuzitengeneza taa zao.
8Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, ‘Tupatieni mafuta yenu kidogo; taa zetu zinazimika.’