38“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’
39Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na la pili pia.
40Kama mtu akitaka kukushtaki na kuchukua joho lako, mwachie achukue na koti pia.
41Kama mtu akikulazimisha kwenda maili moja, nenda naye maili mbili.
42Mpe yeye akuombaye, wala usimgeuzie kisogo yeye atakaye kukukopa.