35Idadi kutoka kabila la Manase walikuwa watu 32,200.
36Kutoka wazao wa Benyamini: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
37Idadi kutoka kabila la Benyamini walikuwa watu 35,400.
38Kutoka wazao wa Dani: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
39Idadi kutoka kabila la Dani walikuwa watu 62,700.