33Idadi kutoka kabila la Efraimu walikuwa watu 40,500.
34Kutoka wazao wa Manase: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
35Idadi kutoka kabila la Manase walikuwa watu 32,200.
36Kutoka wazao wa Benyamini: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
37Idadi kutoka kabila la Benyamini walikuwa watu 35,400.