Hesabu 10

Waliondoka kwa mara ya kwanza kwa agizo la Bwana kupitia kwa Mose.

Numbers 10:13 (UKJV) And they first took their journey according to the commandment of the LORD by the hand of Moses.

11Katika siku ya ishirini ya mwezi wa pili wa mwaka wa pili, wingu liliinuka kutoka juu ya maskani ya Ushuhuda.

12Ndipo Waisraeli wakaondoka kutoka Jangwa la Sinai wakasafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine mpaka wingu lilipotua katika Jangwa la Parani.

13Waliondoka kwa mara ya kwanza kwa agizo la Bwana kupitia kwa Mose.

14Vikosi vya kambi ya Yuda vilitangulia kwanza chini ya alama yao. Nashoni mwana wa Aminadabu alikuwa kiongozi wao.

15Nethaneli mwana wa Suari alikuwa kiongozi wa kabila la Isakari,

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.