Hesabu 16

“Jitengeni kutoka kwenye kusanyiko hili ili nipate kuwaangamiza mara moja.”

Numbers 16:21 (UKJV) Separate yourselves from among this congregation, that I may consume them in a moment.

19Kora alipokuwa amekusanya wafuasi wake wote kuwapinga Mose na Aroni kwenye mlango wa Hema la Kukutania, utukufu wa Bwana ukatokea kwa kusanyiko lote.

20Bwana akamwambia Mose na Aroni,

21“Jitengeni kutoka kwenye kusanyiko hili ili nipate kuwaangamiza mara moja.”

22Lakini Mose na Aroni wakaanguka kufudifudi na kulia kwa sauti, wakasema, “Ee Mungu, Mungu wa roho za wanadamu wote, utakuwa na hasira na kusanyiko lote wakati ni mtu mmoja tu ametenda dhambi?”

23Ndipo Bwana akamwambia Mose,

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.