19Mtawala atakuja kutoka kwa Yakobo na kuangamiza walionusurika katika mji.”
20Kisha Balaamu akawaona watu wa Amaleki, na kutoa ujumbe wake: “Amaleki ilikuwa ya kwanza miongoni mwa mataifa, lakini mwisho wake itaangamizwa milele.”
21Kisha akawaona Wakeni, akatoa ujumbe wake: “Makao yenu ni salama, kiota chenu kiko kwenye mwamba.
22Hata hivyo ninyi Wakeni mtaangamizwa Ashuru atakapowachukua mateka.”
23Ndipo akatoa ujumbe wake: “Lo, ni nani atakayeweza kuishi wakati Mungu atakapofanya hili?