Hesabu 27

Ikiwa hana binti, wape ndugu zake wa kiume urithi wake.

Numbers 27:9 (UKJV) And if he have no daughter, then all of you shall give his inheritance unto his brethren.

7“Wanachosema binti za Selofehadi ni sawa. Ni lazima kwa hakika uwape milki kama urithi miongoni mwa ndugu za baba yao, na kubadili urithi wa baba yao uwe wao.

8“Waambie Waisraeli, ‘Ikiwa mtu atakufa naye hakuacha mwana, utampa binti yake urithi wake.

9Ikiwa hana binti, wape ndugu zake wa kiume urithi wake.

10Ikiwa hana ndugu wa kiume toa urithi wake kwa ndugu za baba yake.

11Ikiwa baba yake hakuwa na ndugu wa kiume, toa urithi wake kwa ndugu wa karibu katika ukoo wake, ili aumiliki. Hili litakuwa dai la sheria kwa Waisraeli, kama Bwana alivyomwamuru Mose.’ ”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.