1Bwana akawaambia Mose na Aroni,
2“Wahesabu Wakohathi walio sehemu ya Walawi kwa koo zao na jamaa zao.
3Wahesabu wanaume wote wenye umri wa miaka thelathini hadi hamsini wanaokuja kutumika katika kazi ya Hema la Kukutania.
4“Hii ndiyo kazi ya Wakohathi katika Hema la Kukutania: Watatunza vitu vilivyo vitakatifu sana.