1Waraka wa Paulo na Timotheo, watumishi wa Kristo Yesu: Kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu walioko Filipi, pamoja na waangalizi na mashemasi:
2Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi.
3Ninamshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo ninyi.
4Katika maombi yangu yote daima nimekuwa nikiwaombea ninyi nyote kwa furaha,