20Sina mtu mwingine kama yeye, ambaye ataangalia hali yenu kwa halisi.
21Kwa maana kila mmoja anajishughulisha zaidi na mambo yake mwenyewe wala si yale ya Yesu Kristo.
22Lakini ninyi wenyewe mnajua jinsi Timotheo alivyojithibitisha mwenyewe, kwa maana ametumika pamoja nami kwa kazi ya Injili, kama vile mwana kwa baba yake.
23Kwa hiyo, ninatumaini kumtuma kwenu upesi mara nitakapojua mambo yangu yatakavyokuwa.
24Nami mwenyewe ninatumaini katika Bwana kwamba nitakuja kwenu hivi karibuni.