Wafilipi 4

Nawasihi Euodia na Sintike wawe na nia moja katika Bwana.

Philippians 4:2 (UKJV) I plead to Euodias, and plead to Syntyche, that they be of the same mind in the Lord.

1Kwa hiyo, ndugu zangu, ninaowapenda na ambao ninawaonea shauku, ninyi mlio furaha yangu na taji yangu, hivi ndivyo iwapasavyo kusimama imara katika Bwana, ninyi wapenzi wangu.

2Nawasihi Euodia na Sintike wawe na nia moja katika Bwana.

3Naam, nakusihi wewe pia, mwenzangu mwaminifu, uwasaidie hawa wanawake, kwa sababu walijitaabisha katika kazi ya Injili pamoja nami bega kwa bega, wakiwa pamoja na Klementi na watendakazi wenzangu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima.

4Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini!

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.