Mithali 1

mimi nami nitawacheka katika maafa yenu, nitawadhihaki wakati janga litawapata:

Proverbs 1:26 (UKJV) I also will laugh at your calamity; I will mock when your fear comes;

24Lakini kwa kuwa mlinikataa nilipowaita na hakuna yeyote aliyekubali niliponyoosha mkono wangu,

25kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote na hamkukubali karipio langu,

26mimi nami nitawacheka katika maafa yenu, nitawadhihaki wakati janga litawapata:

27wakati janga litawapata kama tufani, wakati maafa yatawazoa kama upepo wa kisulisuli, wakati dhiki na taabu zitawalemea.

28“Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu; watanitafuta lakini hawatanipata.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.