29Kwa kuwa walichukia maarifa, wala hawakuchagua kumcha Bwana,
30kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu, na kukataa maonyo yangu,
31watakula matunda ya njia zao, na watashibishwa matunda ya hila zao.
32Kwa kuwa ukaidi wa wajinga utawaua, nako kuridhika kwa wajinga kutawaangamiza.
33Lakini yeyote anisikilizaye ataishi kwa usalama, atatulia, bila kuwa na hofu ya madhara.”