27wakati janga litawapata kama tufani, wakati maafa yatawazoa kama upepo wa kisulisuli, wakati dhiki na taabu zitawalemea.
28“Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu; watanitafuta lakini hawatanipata.
29Kwa kuwa walichukia maarifa, wala hawakuchagua kumcha Bwana,
30kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu, na kukataa maonyo yangu,
31watakula matunda ya njia zao, na watashibishwa matunda ya hila zao.