21Hakuna dhara linalompata mwenye haki, bali waovu wana taabu nyingi.
22Bwana anachukia sana midomo idanganyayo, bali hufurahia watu ambao ni wa kweli.
23Mtu mwenye busara hujihifadhia maarifa yeye mwenyewe, bali moyo wa wapumbavu hububujika upumbavu.
24Mikono yenye bidii itatawala, bali uvivu huishia katika kazi za utumwa.
25Moyo wa wasiwasi humlemea mtu, bali neno la huruma humfurahisha.